GET /api/v0.1/hansard/entries/1444145/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1444145,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444145/?format=api",
"text_counter": 256,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "moja hadi nyingine ilhali wanalipa kodi. Naunga mkono kwamba watengewe sehemu za kufanyia biashara. Sehemu ambazo wanafanyia biashara ziwe na huduma zinazohitajika. Kuwe na vitu kama vile vyoo kwa sababu ni watu wanaofanya biashara zao kwa muda mrefu hadi usiku. Tumesema kwamba tunataka uchumi unaondeshwa masaa 24. Hilo litawezekana ikiwa wachuuzi hao watashughulikiwa. Sehemu kama hizo zinafaa kuwekwa taa. Kwa lugha ya mtaani, wanasema “mulika mwizi.” Staki kusema hivyo kwa sababu yatakuwa maendeleo. Tunafaa kuwa na taa za kumulika maendeleo. Si hayo tu. Ukitembea sehemu nyingi, utapata kuwa wachuuzi hawakutiliwa maanani na kaunti zetu. Kama alivyosema Sen. Ogola, kwa mfano, ukienda mahali panaitwa Naibor, utapata vibanda ambavyo vingetumika na wachuuzi havina mtu yeyote kwa sababu hawakuhusishwa. Ukienda Sosian, hali ni hiyo hiyo. Pesa ambazo tunapigania sisi kama Seneti kuhakikisha zinapelekwa katika kaunti zetu zinatumiwa lakini kwa sababu wafanyibiashara hawakuhusishwa, wanasema mahali ambapo vibanda vimejengwa ni mbali na wateja wao. Kama Sen. Okenyuri anavyopendekeza kwamba kuwe na sehemu hizo, itajulikana kwamba kila mtu anayefanya biashara anafaa kuenda pale. Hakutakuwa na ushindani mkali kusema kwamba yule yuko karibu na mjini na huyu ameondolewa. Lazima mtu awe na barua ikiwa ni mchuuzi wa rejareja na anafanyia biashara yake mahali ambapo hapajatengwa. Hiyo inamaanisha kwamba wote wataenda mahali pamoja. Ukienda mahali panaitwa Sipili, Jumamosi ndio siku iliyotengwa kwa wachuuzi kufanya kazi. Hata hivyo, mahali pale hapana choo. Ijapokuwa wanafanya kazi zao, huduma zingine zinazohitajika haziko. Sio pale pekee. Kuna pahali panaitwa Gatundia. Jumapili ndio siku ya soko na shida ni ile ile. Pahali pengine ni Muthengera. Ijumaa ndio siku ya soko na shida ni ile ile. Ukienda Rumuruti siku ya Alhamisi wakati ng’ombe wanauzwa, mahali pale hapana choo wala huduma yoyote."
}