GET /api/v0.1/hansard/entries/1444146/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1444146,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444146/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Mswada huu ukipitishwa utatoa mwongozo vile sehemu ikitengwa, ni nini kinapaswa kuwekwa pale ili wachuuzi wetu wanufaike. Hii pia inatatua ule ushindani ulioko. Unapata mchuuzi anauza bidhaa zilizosawa pale nje kwa duka ya mfanyibiasha aliyepangisha nyumba. Si sawa kwa sababu huu ni ushindani usio mzuri. Kwa hivyo, kutengwa kwa sehemu hizi kutasaidia ili kila mtu apate riziki yake. Imesemwa na ningependa kurudia, hii kazi ya uchuuzi inafanywa na vijana na watu wasio na hela nyingi. Mara nyingi unasikia unapoenda kutafuta kazi yoyote unaulizwa kama uko na ujuzi au uzoefu. Hizi sehemu zikitengwa na mtu aanzie hii kazi ya rejareja pale hata kwa Shilingi elfu mbili au elfu tuatu, atakuwa na uzoefu wakati atafungua duka au biashara kubwa. Atakuwa pia amejua ni biashara nyingine gani anaweza kufanya na ikampa faida."
}