GET /api/v0.1/hansard/entries/1444148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1444148,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444148/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Kwa kuangazia, Mswada huu uliwasilishwa na Sen. Esther Okenyuri. Sisi kama Chama cha United Democratic Alliance ( UDA) ambacho Okenyuri ni mwanachama, tulipokuwa tunafanya uchaguzi, tulisema tutazingatia wale walioko chini kama vile mama mboga, watu wa boda boda na vinyozi. Hivyo basi, nampongeza kwa sababu Mswada huu umelenga papo ndipo kwa kuwashughulikia vilivyo. Kwa hivyo, mimi niko na kila sababu kuunga mkono Mswada huu. Ukitembelea sehemu nyingi za Laikipia na Nyahururu, shida kubwa wanayopata wachuuzi wetu ni ukosefu wa sehemu za kuuzia."
}