GET /api/v0.1/hansard/entries/1444159/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1444159,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444159/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okenyuri",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nawapongeza Maseneta waliochangia Mswada huu kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Biashara na Viwanda, Seneta wa Kajiado, Sen. Seki. Nimesikia mawazo yako na nitaongezea yale uliyoyasema. Pia, dadangu, Sen. Tabitha Mutinda, shukrani kwa hoja zako. Shukrani pia kwa Seneta wa Tana River almaarufu Seneta Mla Mamba, Sen. Mungatana. Asante sana kwa kisa ulichosimulia hasa ukiwa katika shule ya upili. Nimesikia mawazo yako ya kunipa motisha katika Mswada huu. Pia, nampongeza Seneta wa Makueni, Sen. Maanzo. Amechangia kwa kusema, Mswada huu utawapa ajira vijana wasio na kazi katika jamii."
}