GET /api/v0.1/hansard/entries/1444161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1444161,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444161/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okenyuri",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nikimalizia, ninajua Maseneta wengi wangependa kuzungumzia Mswada huu lakini kwa sababu ya muda, hawa ambao wamezungumza wameweza kutoa mawazo bora bila kumsahau Seneta wa Laikipia, Sen. Kinyua ambaye pia amegusia mambo ya kwa nini Waziri ametajwa kwenye Mswada huu mno. Hii ndio sababu Mswada huu umekuja kwenye Bunge ili tujadiliane na kuuboresha. Kwa hivyo, Sen. Kinyua nimesikia hoja zako katika kuchangia Mswada huu na ninatoa ahadi kuwa haya yote tutayazingatia ili tuweze kutunga sheria ambazo zinawanufaisha wananchi ambao tunawaongoza."
}