GET /api/v0.1/hansard/entries/1444162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1444162,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444162/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okenyuri",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mambo ya uchuuzi hayafanyiki Kenya tu ama kwa mataifa ambayo yanayoendelea pekee, lakini yanafanyika hata kwa yale mataifa ya Ugaibuni. Ukienda kama Marekani, Uingereza, Afrika Kusini na kwa wenzetu hapa Afrika Mashariki kama vile Tanzania na Uganda, kuna wachuuzi katika sehemu hizo zote. Itambulike kuwa wachuuzi hawajisaidi wao wenyewe. Wakati wanafanya biashara hizi zao ndogo ndogo, wanajisaidia na kusaidia familia zao ambazo wamekuwa nazo."
}