GET /api/v0.1/hansard/entries/1444167/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1444167,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444167/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Okenyuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Vile vile, Mswada huu ulikuwa unagusia mambo ya wale askari kwenye kaunti ambao kwa lugha ya mtaa wanaitwa “kanjo”. Mswada huu pia unaangazia wachuuzi hawa wadogo wadogo wasiweze kudhulumiwa na watu kama hao. Ikiwa watadhulumiwa, kuna njia ambazo mambo haya yataweza kuangaliwa. Kwa sababu ya muda sitaweza kuyataja haya yote lakini nimefurahishwa sana na mchango wa wale Maseneta ambao waliochangia Mswada huu pamoja na mchango wa wale ambao tumekuwa tukishirikiana nao sana sana kwenye Kamati ya Biashara na Fedha."
}