GET /api/v0.1/hansard/entries/1445819/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1445819,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1445819/?format=api",
"text_counter": 213,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti kuhusu miradi ya kujenga makao makuu ya kaunti za Lamu, Tana River, Tharaka-Nithi, Isiolo na Nyandarua. Miradi hii ilianzishwa katika awamu ya kwanza ya serikali za kaunti. Sasa hivi tuko katika awamu ya tatu lakini miradi hiyo haijakamilika. Hiyo inamaanisha kwamba muda mrefu umepita na rasilimali nyingi zimepotea kwa sababu ya kuchelewesha ukamilishaji wa miradi hiyo. Ripoti hii ni ya kuungwa mkono kwa sababu inanuia kusimamisha utepetevu ambao umekuwa ukiendelea na kuchangia kutokamilishwa kwa miradi hiyo. Ikumbukwe kwamba Serikali ilikuwa imejitolea kulipa asilimia 70 ya miradi hiyo na kaunti husika zilipe asilimia 30. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}