GET /api/v0.1/hansard/entries/1445820/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1445820,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1445820/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Ukisoma Ripoti hii, utapata kuwa Serikali ndio imechelewesha ukamilishaji wa miradi hiyo. Sababu ni kwamba wakati serikali za kaunti zilikuwa zinatoa michango yao wa asilimia 30, Serikali ya Kitaifa ilikuwa inashindwa kupeleka pesa hizo kwa wakati, hivyo basi kusababisha ucheleweshaji wa miradi hiyo. Katika sehemu nyingine, Gavana wa Tana River alikataa kuhudhuria vikao kadha vya Kamati ya Fedha na Bajeti ambavyo vilikuwa vimeitishwa ili kusuluhisha swala hili. Nakumbuka tulikuwa na kikao kimoja katika Hoteli ya Jacaranda ambapo Naibu wa Gavana ndiye aliyekuja. Alipoulizwa amekuja kwa mkutano gani, alisema kuwa alikuwa amesikia kuna mkutano na kwa hivyo akaja kuhudhuria. Mbali na kwamba kulikuwa na utepetevu katika Serikali ya Kitaifa, baadhi ya kaunti zetu pia zilikuwa na utepetevu kwa sababu hawakuwa tayari kuendeleza miradi hiyo bila mchango wa Serikali ya Kitaifa. Kamati imependekeza kwamba kaunti hizo zichukue miradi hiyo na kuhakikisha imekamilika kwa kutumia pesa ambazo Serikali ya Kitaifa ilikuwa imetenga. Pesa hizo ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya miradi hiyo zipelekwe huko kwa haraka ili isicheleweshwe tena. Nawaomba Maseneta wote tuunge mkono mapendekezo haya kwa sababu yatasaidia kuhakikisha kwamba miradi hiyo ambayo imekuwa kwa zaidi ya miaka kumi imekamilika. Kuna kaunti ambazo zilianza kujenga makao makuu baadaye na zikakamilisha wakati hizi kaunti tano bado zinasubiri ukamilishaji wa miradi hiyo. Iwapo miradi hiyo itakamilika, kaunti hizo zitaweza kuhudumia watu wao kwa njia nzuri zaidi kuliko wanavyofanya sasa. Kwa mfano, wakati wa Seneti iliyopita, tulikwenda katika Kaunti ya Isiolo. Tulikutana na maafisa wakuu wa kaunti hiyo katika canteen ya polisi pale Isiolo. Hakukuwa na mahali pengine ambapo wangeweza kukutana na Maseneta na kujadili matatizo katika kaunti hiyo. Hali hiyo ni ile inayojulikana kwa Kiingereza kama wake up call . Kaunti zetu zinafaa kujisimamia. Kuna maswala mengine ambayo hawawezi kuyaacha kwa muda huo wote kama vile makao makuu ya kaunti hizo. Kwa mfano, kule kwetu Mombasa, kuna mradi wa Mombasa Municipal Stadium. Ni karibu miaka mitano lakini mradi huo haujakamilika kwa sababu fedha ambazo zilitengwa hazikupatikana. Kwa miaka miwili sasa, serikali mpya ya kaunti haijatenga pesa za kutosha kuhakikisha kwamba mradi ule unakamilishwa. Juzi nilikuwa nasoma ripoti ya Mkaguzi Mkuu ya Mwaka 2022/2023. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba Ksh600 milioni za Kaunti ya Mombasa hazikuwa zimetumika kufikia tarehe thelathini mwezi wa sita mwaka uliokwisha. Hatujui zitabakia ngapi katika ripoti ya mwaka huu. Kama Ksh600 milioni ambazo hazikutumika mwaka jana zingepelekwa katika mradi wa Mombasa Municipal Stadium, mradi huyo ungekuwa umesonga mbele sana. Serikali za kaunti haziwajibiki kukamilisha miradi ambayo ilianzishwa na magavana waliotangulia. Hiyo haifanyiki kule Mombasa pekee bali kaunti zote. Kwa mfano, mwaka jana, tulizuru mradi mmoja wa ECDE sehemu za Chaani katika Kaunti ya Mombasa. Gavana aliahidi kwamba atakamilisha mradi ule kabla ya mwaka kukamilika. Mwaka ulikamilika juzi tarehe 30 Mwezi wa Sita, ilhali mradi huo bado hujakamilika. Kwa hivyo, zipo cheche chini kwa chini ambapo magavana wapya wakichaguliwa, hawana nia au mvuto wa kukamilisha miradi ambayo ilianzwa na serikali zilizotangulia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}