GET /api/v0.1/hansard/entries/1446001/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1446001,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446001/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Mhe. Spika. Jana tulipoanza mazungumzo ya Hoja hii, nilisema ya kwamba pesa nyingi za neti za mbu zilifujwa kutoka Global Fund zilifujwa, ambazo zilipotea katika Wizara ya Afya. Wakati huo, tarehe kuni na tano, Mwezi wa Tano, Mkuu wa Utumishi wa Umma, Bw. Felix Koskei, alitoa matamshi ama statement, ambayo walichukua hatua kama Serikali kuu. Aliyekuwa Principal Secretary wa Afya alifutwa kazi. Halmashauri ya Kenya Medical Supplies Authority (KEMSA) ilivunjwa na wafanyakazi waliohusika waliondolewa kutoka halmashauri ya KEMSA na wakapewa transfer kwenda sehemu zingine."
}