GET /api/v0.1/hansard/entries/1446006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1446006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446006/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, hiyo kazi ilifanyika miezi tisa baada ya uchaguzi wa Serikali ya Rais Dkt. William Ruto. Kulikuwa na msisimko na halijoto ya watu kutaka kufanya kazi. Kulikuwa na mwito kwamba wafanyakazi wa Serikali wafanye kazi yao kwa haki. Haya yananikumbusha wakati Serikali ya Rais Mwai Kibaki ilipochaguliwa mara ya kwanza. Wananchi walikuwa wamejitolea kabisa kwamba kutakuwa na mageuzi na usimamizi mpya wa pesa zetu. Nakumbuka wakati huo, hata polisi wakiitisha hongo barabarani, wananchi watukufu walikuwa wanashuka na kumwambia polisi kuwa hawataki achukue hongo kwani basi lao halikuwa na makosa. Wananchi walikuwa na msisimko mkubwa wakati huo tulipoingia Serikali ya muhula wa kwanza wa Rais Mwai Kibaki. Miezi tisa ya kwanza ya muhula wa Rais Dkt. William Ruto, Serikali bado ilikuwa na ule moto wa kugeuza mambo. Lakini juzi, miaka miwili baada ya sisi kuwa mamlakani, vijana wamejitokeza barabarani na kusema ya kwamba kuna ubadhirifu wa pesa, utumizi mbaya na hali mbaya ya usimamizi wa pesa."
}