GET /api/v0.1/hansard/entries/1446008/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1446008,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446008/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu Spika, Serikali hii imekumbushwa kuwa wananchi watukufu wanataka usimamizi mzuri wa pesa za umma. Kuna mengi mabaya yaliyofanyika lakini kuna point muhimu ambayo imewekwa katika maandamano yaliyofanywa na vijana; kwamba wanataka kuona usimamizi mzuri wa fedha zetu. Uzuri wa maandamano haya ni kuwa hayakusimama hapa wala yaliwafikia magavana hadi kwenye kaunti. Walisema wanataka usimamizi mzuri wa fedha hata katika sehemu gatuzi za nchi yetu."
}