GET /api/v0.1/hansard/entries/1446083/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1446083,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446083/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono ripoti maalum ya ujumbe wa Bunge la Seneti katika Kikao cha 66 cha mkutano wa Commonwealth mjini Accra, Ghana. Jumuia ya Commonwealth ni moja katika jumuia za ulimwengu ambazo zimestawi kwa muda mrefu. Imeweza kujumuisha nchi ambazo zilitawaliwa na Waingereza wakati wa ukoloni. Kama alivyotangulia kusema, Sen. (Prof.) Kamar, ujumbe huu uliongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa, Mheshimiwa Wetangula. Upande wa Seneti, kiongozi wetu wa ujumbe alikuwa ni Sen. (Prof.) Kamar. Pamoja na Sen. Wamatinga, sote tulihudhuria na kushiriki pakubwa katika vikao pamoja na mijadala tofauti tofauti iliyoendelea katika mkutano huo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}