GET /api/v0.1/hansard/entries/1446084/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1446084,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446084/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Ripoti ni nzuri sana na imetoa kwa ufasaha zaidi mambo yale ambayo yalijadiliwa katika mkutano huo na zile nususi ambazo zilihusika katika mkutano huo. La msingi ni kuwa maazimio haya ambayo yamezungumziwa katika ripoti hii, yote yalikubaliwa pamoja na zile jumbe nyingine zote ambazo zilihudhuria mkutano huo. Ningependa kuguzia kwamba kulikuwa mijadala kuhusiana na ugaidi kama tishio kwa nchi. Suala hili ni muhimu sana kwa sababu hapa Kenya, tumepigwa mara kwa mara na makundi ya kigaidi. Kwa mfano, bomu lililipuliwa katika Ubalozi wa Marekani hapa Nairobi, mashambilio ya Garissa University na vile vile mashambulio ya Dusit2 Hotel na mengineyo mengi ambayo yamefanyika katika nchi yetu kutokana na ugaidi. Tuliweza kujadili mbinu tofauti tofauti za kuzuia ugaidi pamoja na itikadi kali kwa sababu, mambo haya mawili yanaingiliana. Mtu ataanza katika itikadi kali na baadaye anaingia katika ugaidi. Tulisema kwamba, ni lazima kuwe na ushirikiano baina ya mataifa kwa sababu, mara nyingi magaidi wanafanya njama zao katika nchi tofauti tofauti. Kwa mfano, hapa Kenya, mashambulizi mengi ambayo yametokea, magaidi wengi wametoka katika upande wa Al-shabab kutoka nchi ya Somalia. Kwa hivyo, ipo haja ya nchi ambazo ni jirani zetu kushirikiana kuhusiana na kutambua na vile vile kukinga mambo ya ugaidi. Suala lingine ni kwamba ni lazima kutolewe rasilmali ya kutosha ya kupambana na ugaidi pamoja na kununua vifaa vya kisasa vya kutambua silaha hatari ambazo zinaingizwa katika nchi zetu. Vile vile ushirikiano na makundi ya kijamii; the civilsociety organizations, ili kupeleka ujumbe kwamba ugaidi ni jambo ambalo linaharibu nchi na linasababisha maafa. Tulisema kuwa, ipo haja ya kuyapa nafasi Mabunge ili yaweze kupambana na ugaidi pia. Kwa mfano, iwapo Mabunge yetu yataweza kufanya kazi zake za uangalizi kwa uangalifu, itasaidia pakubwa kujua ni pesa ngapi ambazo zimeenda katika kila eneo. Vile vile zinatumika vipi na zimesaidia vipi kupunguza umasikini, kuimarisha elimu. Pia, kupeleka vitu ambavyo vitaweza kuzuia wananchi kufikiria ya kwamba wametengwa na jamii na vile vile kuingia katika mikono ya wale ambao wanadhamini ugaidi. Vile vile, ni lazima kuwe na sheria ya kuzuia cross border terrorism . Kwa mfano, iwapo gaidi ameingia kutoka nchi jirani, anapofika Kenya, hata kama hajafanya ugaidi, basi sheria iweze kumchukulia hatua kwa hakika ili kupunguza mambo kama hayo. Mambo mengine ambayo yalikuwepo ni masuala ya mazingira na ni vipi tutaweza kuangalia masuala ya umasikini katika kawi yaani Energy poverty. Hili ni suala nyeti kwa sababu katika Afrika bado jamii kubwa inatumia zile kawi za kizamani. Kwa mfano, jamii nyingi hapa Kenya vile vile wanatumia kuni. Utumiaji wa kuni unachangia kuharibu mazingira kwa sababu miti huchukua muda mrefu kukua. Matumizi ya kuni huathiri kile kinachojulikana kwa Kiingereza kama"
}