GET /api/v0.1/hansard/entries/1446328/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1446328,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446328/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa fursa hii. Nimesikiza kwa makini sana Maseneta wenzangu wakichangia Mswada huu muhimu. Nampongeza Seneta wa Kaunti ya Kakamega, Sen. (Dr.) Khalwale, ambaye ni shupavu. Amewahi kufanya kazi katika kaunti yetu ya Kwale na tunamshukuru kwa huduma zake wakati ule. Ndiposa anajiita lile jina ‘Bullfighter.’ Nimetohoa na naomba kwa fursa na heshima kuu niruhusiwe. Mswada huu ni muhimu sana hususan ukizingatia kuwa vijana wengi katika nchi hii wako katika sekta hii ya boda boda. Kwa muda mrefu sekta hii imewachwa wazi. Hakujakuwa na hatua yeyote ya kujaribu kuhakikisha sekta hii pamoja na vijana wameletewa sheria, muundo au mfumo ambao utadhibiti utendakazi ule katika sekta ile. Vijana wengi wamepoteza maisha yao kwa sababu ya kutojali hali yao ya usalama, kutokuwa na mafunzo au nidhamu katika sekta na biashara hii. Seneta wa Kaunti ya Murang’a, Mhe. Joe Nyutu, amenena kuwa utapata kijana anayefahamu kuendesha baiskeli na amemaliza chuo kikuu au shule ya upili na kwa bahati mbaya ameshindwa kutafuta karo ya kusonga mbele, ameamua kujileta katika biashara hii ya boda boda. Kwa dakika chache, kwa sababu anafahamu kuendesha baiskeli, anapata fursa ya kujifunza na kuwa mwana"
}