GET /api/v0.1/hansard/entries/1446330/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1446330,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446330/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mwisho wa siku anakosa nidhamu na mafunzo, na tunampoteza aidha kwa ajali mbaya au matukio yasiyopendeza katika sekta hii. Namshukuru Sen. (Dr.) Khalwale kwa hatua yake ya kudhibiti sekta hii. Vile vile, nawahimiza vijana wenzangu kuwa wakati umefika sasa kujipanga katika biashara hii. Nimeona kuwa kuna pendekezo la vijana wa boda boda kuungana katika Savings and Credit Cooperative (SACCO). Sisi viongozi mara nyingi hususan tukiwa mashinani ninapotoka, Kaunti ya Kwale, huwa ninapokea maombi kutoka kwa vijana wakitamani angalau niwanunulie boda boda ili wapate ajira na kujikimu katika maisha. Nawaeleza kuwa suluhu ya boda boda ipo katika sheria hii ya Sen. (Dr.) Khalwale. Sheria hii inampa fursa kijana kutoka Kaunti ya Kwale, Tana River, Kakamega au Samburu kuwekeza katika boda boda. Juzi niliona vijana wa boda boda katika mji wa Thika, ambao walikuwa wamekuja pamoja, wakaungana na kuwekeza savings zao, wakafikia kununua shamba na kujenga nyumba ambazo wanakodi. Sasa wanapata pato la kuridhisha. Nina imani tukipanga vijana hawa katika SACCO zetu, watapata mapato bora ambayo yatawapatia afueni katika maisha yao. Kwa kifupi, nataka kuzungumzia pendekezo la kuwa na mkataba baina ya mwenye"
}