GET /api/v0.1/hansard/entries/1446335/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1446335,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446335/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Pengine mtanipa jina la Kiswahili. Tayari bei ya kununua pikipiki iko juu. Tukiweka pendekezo kuwa pikipiki iwe na chombo ambacho kinaweza kufuatwa ikiwa imepotea, bado ni gharama kwa mwenye boda boda. Jambo hili litaongeza gharama zaidi ya kupata kifaa kile ili mwenye boda boda aweze kufanya biashara. Ombi langu ni kuwa ikiwa tutaweza tulitupilie mbali pendekezo lile ili pikipiki zetu zipatikane kwa njia ya afueni na kwa bei ya rahisi, ili vijana wetu wafanye biashara yao bila gharama yeyote. Nachukua fursa hii kumpongeza Sen. (Dr.) Khalwale. Naunga mkono sheria hii na mapendekezo ya marekebisho kidogo ndio vijana wetu wa boda boda wapate sheria mwafaka ya kuwapa fursa ya kufanya biashara yao bila bugdha. Asante."
}