GET /api/v0.1/hansard/entries/1446573/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1446573,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446573/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nitoe mawazo yangu kuhusu Mswada huu unaopitisha sheria inayosema kwamba kila mtu anayewekeza kwa sekta ya kuchimba madini, ahakikishe ya kwamba wananchi wa kawaida wa sehemu hiyo wanapata nafasi yakujiendeleza. Jambo la kwanza ni kuwa sielewi kwa nini Mswada huu unaongelea kuhusu mafuta na gesi yanayotolewa ardhini peke yake. Napendekeza jina la Mswada huu ligeuzwe ili lijumuishe wawekezaji wote wanaochimba madini kutoka ardhini. Nasema hivi kwa sababu Mswada huu ni mzuri. Mama Spika wa Muda, ukiangalia sehemu ya Charidende na Bangali kule Tana River, kuna madini yanayotumika kutengeneza cement . Madini haya yanayotwa gypsum na yanatoka sehemu hiyo ya Tana River. Ikiwa wawekezaji wangekuwa wanafuata mapendekezo ya Mswada huu, basi jambo lingewafaidi sana---"
}