GET /api/v0.1/hansard/entries/1446591/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1446591,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446591/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, kule kwetu, sehemu ya Chardende, sheria inayopendekezwa katika Mswada huu ingetufaa sawasawa kama inazungumzia juu ya madini yote pamoja na gesi au mafuta. Kwa hivyo, nimesema ninamkosoa Seneta mwenzangu na ningeomba wakati wa marekebisho ya Mswada huu, tubadilishe jina lake ili kujumuisha madini ya aina yote yanayochimbwa ardhini. Vipengele vyote vilivyo katika Mswada huu vikitekelezwa wakati huu tunachimba jasi, wananchi wetu wangepata manufaa zaidi. Bi. Spika wa Muda, nimefurahi sana ukiangalia Kipengele cha 22. Kinasema kwamba kila mwekezaji atakayekuja kuweka mali yake ni lazima atengeneze mipango kamili kabla hajapewa leseni. Ni lazima aeleze jinsi gani wananchi wa sehemu hiyo kunakochimbwa madini watakavyofaidika. Ukiangalia wale wanaochimba jasi sehemu ya Charidende na kwingineko Tana River, hakuna manufaa wananchi wa kawaida wanapata. Kwa hivyo, ninaunga kipengele The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}