GET /api/v0.1/hansard/entries/1446592/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1446592,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446592/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "hichi cha Mswada huu mkono. Kwa sababu, tungependa wawekezaji wote kabla hawajapewa leseni na kaunti, wawe na mipangilio kamili inayosema kwamba mwananchi wa sehemu hio, atafaidika namna gani. Kipengele cha 26 kimenipendeza sana kuhusu Mswada huu. Kinasema ni lazima mwekezaji aweze kuweka mipangilio kamili ya kusema wananchi wa pale watapata kufundishwa namna ya kuchimba yale madini na kuongeza ujuzi. Wakati huu watu wetu wa sehemu zote ambapo kuna madini yanayochimba hawana ujuzi wa kufanya kazi hiyo wao wenyewe. Bi. Spika wa Muda, watu wanatoka nje, wanakuja wanachimba madini, watu wanaambiwa tu, chimbeni ila hawafundishwi ujuzi kamili. Kusema ukweli wakiyachimba madini pale, sisi tunabaki na mashimo peke yake. Hatubaki na ujuzi unaotakikana tubaki nao. Bi. Spika wa Muda, sheria hii ninayounga mkono inasema katika Kipengele cha 29, kuwa mtu yeyote ambaye ni mwekezaji ama anachimba madini ni lazima aweke mpangilio kamili wa watu wangapi atakaoajiri kazi katika matarajio yake. Kusema ukweli sheria hii imesema na kulenga ndipo. Tukipitisha sheria hii na tuweke mabadiliko, wananchi wetu haswa wa sehemu tunazochimba madini kama kwetu Kaunti ya Tana River watafaidika sana, kwa sababu kwa wakati huu watu wetu hawapati chochote. Wanaajiriwa kazi zisizoeleweka na hawapati ujuzi wowote. Hakuna mipango kamili ya mwananchi kupata manufaa yeyote. Wawekezaji hawa wanapoondoka tunabaki na mashimo ambayo mbuzi na ng’ombe wetu wanaanguka ndani. Bi. Spika wa Muda, sheria hii inasema kabisa kwamba imejihusisha na mambo ya"
}