GET /api/v0.1/hansard/entries/1446594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1446594,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446594/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "katika Katiba ya Kenya. Inasisitiza vile wananchi wanafaa kutumia na kufaidika kutoka kwa mazingira yao. Wakaazi wa Kaunti ya Tana River wanatumiwa vibaya na wawekezaji wanaochimba madini. Naiunga mkono sana sheria hii. Katika kaunti hii, sio Gypsum pekee inachimbwa. Wakati Waziri Mhe. Mvurya, aliondoka katika Wizara ya Madini, alizuru kaunti yangu na kutueleza kwamba kuna map ambayo imechorwa na Serikali. Kaunti ya Tana River ina madini ya kutosha lakini bado hawajapata wawekezaji. Jambo hili linaonyesha kwamba wakati ujao kutakuja wawekezaji wa kutosha sehemu yetu ya Tana River, na wakija tunataka sheria hii itekelezwe. Wakati huo tutapendelea vipengele hivi ambavyo vinasema wananchi wa kawaida lazima waajiriwe kazi, wapewe"
}