GET /api/v0.1/hansard/entries/1446597/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1446597,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446597/?format=api",
    "text_counter": 216,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ambaye pengine atasema anahitaji mkataba kwa sababu unalima madini kwenye ardhi au sehemu ambayo iko na title deed au ni imemilikiwa na mababu wake. Haiwezekani. Kama madini yale yametoka kwenye ardhi ya umma, basi lazima tuweke sheria ambazo zitatufaidi. Kwa wakati huu kuna tetesi kwamba katika sehemu ya kaunti ya Kwale ambapo madini ya Titanium yamechimbwa kutosha, migodi ile inafungwa na wawekezaji wako katika safari ya kumaliza yale mapatano. Tetezi lililo Kaunti ya Tana River, sehemu ya Kipini pia ni kuwa katika harakati za upekuaji wamepata madini haya ya Titanium . Bi. Spika wa Muda, madini haya yana value kubwa sana. Ukweli ni kwamba wakaazi wa sehemu hii ya Kipini hawajahusishwa hadi sasa. Sheria hii ingekuwapo, tungetekeleza mikutano ya wananchi ili watu wakusanywe. Nilihudhuria mkutano wa hadhara ambao Waziri Mhe. Mvurya alikuwa pia na wananchi walizungumza kupitia Member of County Assembly (MCA) wao Mhe. Abubakar. Alisema kuwa wananchi wa sehemu ya Kipini wanafaa kuelezwa vizuri kuhusu tetezi hili la ugunduzi wa madini haya ya Titanium . Bi. Spika wa Muda, watu hawa wanaishi kando ya bahari. Wanategemea bahari kwa chakula cha kila siku na pia kwa biashara zao za kujikidhi kimaisha. Wako na wasiwasi kuwa uchimbaji wa madini ukianza basi hali ya mazingira itaharibika na wataishi vipi. Wawekezaji wale wanafaa kutoka huko juu kwenye ofisi za Waziri katika Nairobi City County na waje kwenye serikali ya kaunti, haswa kwa wananchi wa Tana River, ili waongee na waelezee watu hawa wa sehemu ya Kipini. Tunataka kujua ukweli wa mambo. Kama sheria hii inavyosema ni lazima upelelezi wa kutosha ufanyike ili ijulikane kama mazingira yataharibiwa hadi yafikie wakati ambapo hayatatumika tena. Waekezaji wale watachimba migodi hii ya Titanium kama walivyochimba Kaunti ya Kwale. Madini yakiisha kwenye ardhi wataondoka na kuwacha sehemu hii na mashimo yatakayoleta shida kwa sababu wakaazi hawataweza kurudi kule kuvua Samaki juu ya uharibifu wa mazingira haya. Tukipitisha sheria hii, tunataka watu wahusishwe na waelezwe kikamilifu. Natumia nafasi hii ya Seneti kuwambia waekezaji wa Titanium kuwa hatutaki waende huko kupitia ofisi za juu za Serikali wakiwa Nairobi City County. Washuke chini kwa wananchi na tufanye mikutano na wao ili tuwaeleimishe. Kila mtu anataka maendeleo lakini hatutaki maendeleo ambayo yatamuumiza. Hatutaki tuje tuambiwe ya kwamba hii Titanium tunapokuja kuichimbua hautaweza tena kuvua samaki sehemu hiyo. Mazingira yataharibika na hatutaweza tena kulima. Hii ndiyo wasiwasi tuliyo nayo. Bi. Spika wa Muda, mimi nimesimama kusema kwamba sheria hii ya uchimbaji wa madini tunataka tuifanye iwe ya kisawasawa na wananchi wetu wahusishwe kikamilifu. Miaka iliyopita, watu walikuwa wanafanya mambo kiholela. Wanaenda kufanya mipango ambayo wananchi hawahusishwi. Miaka ya sasa na katika mfumo huu wa kisasa, ni lazima wananchi wahusishwe kikamilifu. Mimi ninaunga mkono Mswada huu na inafaa tuupitishe, lakini kabla hatujaupitisha, wale wawekezaji ambao wanataka kufanya kazi ya kutafuta madini chini ya ardhi tafadhali, wapitie hapa Seneti, waone vile tunatarajia mambo yafanyike. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}