GET /api/v0.1/hansard/entries/1451245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1451245,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1451245/?format=api",
    "text_counter": 92,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa wazima moto na uokoaji wa waathiriwa wa mambo ya moto. Majanga ya moto yamekua mengi katika nchi yetu. Tunaona kaunti zetu hazijakua na mipango mahususi ya kupambana na majanga haya. Tumeona visa vya moto vinapotokea, mali na maisha hupotea wakati wa majanga kama haya. Mswada huu umekuja wakati mwafaka kabisa ili kuweka msingi sheria itakayosaidia mambo haya kwa siku za usoni. Tukianza kabisa, ukiangalia kaunti zetu zote, bajeti zao za zima moto ni ndogo sana, wakati huduma inasaidia pakubwa kukitokea dharura, kuokoa maisha na kuokoa mali. Tukiangalia bajeti zetu zote, si Mombasa na Nairobi, hata kuna kaunti zingine hazina wazima moto. Bw. Spika, sheria hii itatoa nafasi nzuri ya kuhakikisha kwamba mambo ya moto yanaangaliwa kwa undani zaidi. Kuna vipengele vingi ambavyo vinatia moyo katika Mswada huu. Ningependa Maseneta wavisome kwa sababu vinaathiri nchi nzima. Sehemu ambazo moto hutokea kwa mara nyingi huwa hazina magari ya kuzima moto ya kutosha. Hapo awali, Kaunti ya Mombasa ilikuwa na gari moja la kuzima moto peke yake. Lakini sasa kumekuwa na maendeleo kidogo na kuna magari zaidi ya sita. Pia, kuna"
}