GET /api/v0.1/hansard/entries/1451264/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1451264,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1451264/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpatia kongole ndugu yetu, Sen. Abass, kwa kutengeneza sheria ambayo ni ya kuzima moto na kuokoa watu wakati wa janga la moto. Sheria hii inaleta mwelekeo mpya. Tumekuwa kwa muda mrefu na nafasi ambazo hazingeweza kukamilika kutengenezwa kwa sheria ambayo itahusikana sana na uzimaji wa moto. Kama tunavyoelewa, kazi ya kuzima moto hivi sasa inafanywa na magavana wa kaunti. Lakini kuna kasoro, ikiwa nitakosoa kidogo, upande wa magavana wetu wanaohusika na kuangalia jukumu hili muhimu sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}