GET /api/v0.1/hansard/entries/1451265/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1451265,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1451265/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Magari ambayo yameletwa katika kaunti zetu ili kutumika kwenye kazi ya kuzima moto yanaonekana yalinunuliwa kitambo na kupakwa rangi kuonekana mapya. Haya magari yaliletwa na kupakwa rangi kwa ofisi za kaunti. Hakuna hata moja iliyojengewa mahali pazuri isipokuwa Mombasa ambapo wako na stesheni ya magari ya kuzima moto pamoja na staff wenye taaluma ya kupigana na moto. Wamewekwa pale ili waweze kutambuliwa mahali wanaweza kupatikana kwa kazi ambazo wanafanya. Bw. Spika wa Muda, mara nyingi tunaona - kwa mfano katika kaunti kama yangu, Kilifi - kwamba wale wanaofanya kazi ya kuzima moto lazima wawe na training. Sio training tu, lazima wafunzwe ili hiyo kazi iwe ni taaluma yao. Wanafaa wapelekwe college inayohusika na mambo ya kuzima moto. Vitu kama hizo vinakosekana. Mtu anaajiriwa kazi na kuambiwa: Utakuwa unazima moto, ukishika pipe unamwaga maji namna hii. Utapata kwamba mara nyingi taaluma ya kuzima moto sio kushika pipe na kumwaga maji tu pale pana moto. Unatakikana ujue upepo unapiga upande gani; unatakikana ujue utasimama wapi ili kutekeleza shughuli iliyokupeleka pale ya kuzima moto au kuokoa maisha ya wale watu ambao wameathirika. Sisi tunajua kuwa kuna hasara hutokea mara kwa mara. Sheria hii imeweza kuangalia matumaini hayo. Kwanza ni kwamba wale tunaowakabidhi kazi hizo katika kaunti, ni jambo la kusikitisha kwamba hatujapata wale wenye taaluma. Tunaajiri tu vijana na kuwaambia mtakuwa mkizima moto. Ningependa kumuuliza ndugu yangu kama tunaweza kugeuza vipengele fulani hapa ndani kuona ya kwamba hawa watu wote ambao wanafanya kazi katika eneo ile wawekwe katika insurance cover kwa sababu ile kazi wanaofanya ni hatari. Unaweza kupanda ngazi ili uende juu ya nyumba kuzima moto ukaanguka na kupata hasara fulani. Ama unaweza kuteleza ukaingia ndani ya huo moto ambao ulienda kuzima. Kwa hivyo, lazima hawa watu wapewe insurance cover ambayo ni kitu muhimu sana kwa wale wanaofanya kazi hii ya kuzima moto. Vile vile, kuna wale wanaofanya hii kazi ambao ni wazembe. Mtu anakuja kazini na kuketi pale anapotakikana kukaa kama dereva. Notisi inapotokea kwamba mnaenda kuzima moto mahali fulani, unapata kwamba huyo mtu hawezi kupeleka ile gari kwa sababu jana alikesha kwenye kilabu akiwa mlevi. Kwa upande mwingine, anaweza kukosa kuja kazini kwa sababu ni mgonjwa. Sababu kama hizo tunazielewa lakini hali ya uvunjaji sheria sio sawa. Unafaa kuwa mtu ambaye watu wako na matumaini kwako kwamba wakati wowote kukitokea janga la moto, wewe unaweza kutokea kwa haraka na kusaidia kuokoa maisha ya watu waliokumbwa na janga hilo. Bw. Spika wa Muda, mara nyingi, moto ukitokea, matumaini ya watu huwa kwa hao wazima moto. Nataka kuzungumzia experience yangu. Miaka mbili iliyopita, nyumba yangu kule upande wa Mtwapa, ilishika moto na kuchomeka. Nilipiga simu, mimi kama Seneta na kusema kwamba ninataka gari ya kuzima moto ije inisaidie lakini hakuna gari hata moja ilikuja. Ilibidi tuende mpaka Mtwapa kuitisha gari na kusema ije haraka sana; hiyo ndio gari iliyofika pale kwangu. Wale vijana walikuja na gari bila kuangalia kama iko na maji. Gari ya kuzima moto ilikuja na iliipofika pale ikawa haina maji. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}