GET /api/v0.1/hansard/entries/1451266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1451266,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1451266/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Magari haya huwa yamenunuliwa mamilioni ya pesa. Lakini, utapata gari limekuja mpaka pale bahari, wakijaribu kufungua, gari lenyewe halifanyi kazi na halina nguvu ya kutoa maji ya kuzima ule moto. Kwa hivyo, jambo kama hili sio la kuchekesha kwa sababu itakuwa hasara. Mimi nilipata hasara kwa kuchomekewa na nyumba. Lakini, nashukuru Mwenyezi Mungu kwani hakuna mtu aliumia. La mwisho, magari haya pia ni lazima yaangaliwe. Mara nyingi utapata katika kaunti zetu, magari ya watu kwenda kutembea au kufanya kazi zao mbalimbali za kaunti, yanapatikana. Lakini, lazima kuwe na sheria mwafaka ambayo ndugu yangu, Sen. Abass, anaweza kuangalia. Magari haya yakitengenezwa, yapewe muda ule yanaweza kutumika kama ni miaka miwili au mitatu ili yaondolewe na magari mengine yaletwe. Hii itawezesha magari yaliyo sawa kufanya kazi. Pia, tuhakikishe magari hayo yako na mafuta na katika hali nzuri. Wakati wowote ukipiga simu usiku ama mchana, yanaweza kupatikana. Naona ugonjwa huo uko katika kaunti zetu. Katika kaunti zetu, unaweza kupiga simu ukaambiwa ungoje wanakuja hadi ule moto uchome na kuteketeza kila kitu kabla ya magari kufika. Itakuwa vyema ikiwa sisi tutazingatia sheria hii ambayo itakuwa na bodi itakayohakikisha sheria zake zimefaulu. Wale wanaohusika na mambo watazingatia sheria hizi za kuzima moto na kuokoa jamii, wananchi ama mali iliyokuwa inapatwa na hasara ya kuteketezwa. Asante."
}