GET /api/v0.1/hansard/entries/1451697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1451697,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1451697/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "s mbili au wasaidiwe vinginevyo. Hazina ya NG-CDF imesaidia na sasa hakuna mtu anayeenda Ikulu. Wabunge wana nafasi ya kusema ukweli wa mambo yalivyo. Kama kuna makosa, watasema hata kama ni kwa kiongozi wa taifa kwa sababu wanajua miradi ya hazina ya NG-CDF itaendelea bila ya kuenda kuomba omba. Naweza kuwaita wachawi au wanga wale wanaopendekeza hazina ya NG-CDF iondolewe. Watu wanasaidika kwa kupata bursaries za shule na pesa za kujifundisha ujuzi. Kazi ya Mbunge ni kuhakikisha kuwa watu anaowakilisha wanapata msaada na ikiwezekana, atafute mbinu ya watu hao kuendelea kupata fedha hizo badala ya kusema hazina ya NG-CDF iondolewe. Huo ni uchawi. Kule mashinani kuna matatizo mengi sana. Ikiwa kuna jambo ambalo Mbunge halitaki, aende akalifanyie public participation. Awaulize wananchi mashinani ikiwa wanahitaji hazina ya NG- CDF iendelee, badala ya kuamua ofisini na kusema hii hazina ikatwe. Haya ndiyo yanayoleta matatizo kama yaliyotokea juzi. Taifa linaongozwa na sheria. Hata kama Mbunge ana uwezo wa kwenda mahakamani, kwanza ni muhimu aulize wananchi ikiwa wanahitaji hazina ya NG-CDF. Sina shida na fedha walizo nazo ndugu zetu katika county governments kwa mfano, governors . Sina shida nao wakitoa bursaries. Bursaries wanazotoa pamoja na hazina ya NG-CDF hupewa mwananchi. Ni vizuri kama itawasaidia wananchi kumaliza masomo bila kero. Watu wetu wana kero. Kuna shida. Fedha ya hazina ya NG-CDF lazima iangaliwe ili matokeo yake yaonekane na hata kama mtu haoni, anaweza akapelekwa akashike matokeo hayo. Hata hivyo, kuna hazina ambazo faida zake hazionekani. Kuna fedha nyingi ambazo watu wamepata lakini hakuna miradi yake inayoonekana. Hii NG-CDF imesaidia na iendelee kusaidia kwa sababu inaipa umakini wale viongozi. Hakuna mtu tutampigia magoti. Tutahakikisha kwamba watoto wanapata usawa. Na hali ilivyo, NG-CDF imekatwa mambo mengi. Kuna vitu kama security lights, unaambiwa kwamba hii usifanye; borehole unaambiwa usifanye. Unakuta ulijenga shule umemaliza, unaambiwa usijenge borehole kwa sababu hiyo si kazi yako. Sasa ile shule inakaa bila maji kwa sababu ya mambo tu madogo madogo. Kwa hivyo, iwekwe wazi, kwa sababu ni hazina ambayo inakaguliwa na inasaidia mwananchi. Mtu asiwe na nia kwamba yeye aitoe, kwa sababu anataka kupunguza matumizi ya pesa. Na kama ni kupunguza matumizi, kuna Bunge la Kitaifa hapa na kuna Seneti. Wacha Seneti ivunjwe, sote tuje hapa tung’ang’ane ili tusave ile pesa. Kama wewe unataka kusimamia mradi huo, mimi nimesimama kuunga mkono NG-CDF iendelee. Ahsante sana."
}