GET /api/v0.1/hansard/entries/1456598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1456598,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456598/?format=api",
    "text_counter": 3988,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nimengojea kwa muda lakini nimepata nafasi. Kwanza, natoa rambirambi zangu kwa familia za wale waliopoteza wapendwa wao wakati wa maandamano. Kenya ni yetu sisi sote na bila amani hatuwezi kuwa na maendeleo. Licha ya kuwa watoto wetu walizungumza mambo mengi na yamesikizwa, nawaomba waweze kutulia. Kama ninavyo ona katika hii bajeti, mambo yao yameangaliwa na yale yaliokuwa yanawasumbua yametolewa."
}