GET /api/v0.1/hansard/entries/1456599/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1456599,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456599/?format=api",
"text_counter": 3989,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Nachukua fursa hii kumpongeza ndugu yangu kipenzi, tunayemuenzi, simba wa Pwani, Hassan Ali Joho, kwa kuwekwa katika ule msururu ambao utakuja kupigwa msasa hapa Bungeni kama Waziri wa Uchumi Samawati na Madini. Nampongeza pia Kinara wangu wa Chama kwa kumkumbatia ndugu yetu na kumweka katika wale ambao wameteuliwa. Kwetu Mombasa ni furaha kubwa na tunajua ni mchapa kazi kwa yale ambayo aliweza kufanya akiwa Mbuge wa Kisauni, Gavana wa Mombasa na Naibu wa Waziri.Ataweza kuboresha uchumi samawati na madini Kenya na kuinua uchumi wa Kenya Mhe. Spika wa Muda. Namuombea mahali popote alipo mwenyezi Mungu amtangulie mbele na naomba Wabunge wenzangu, akija hapa Bungeni, tuweze kumpa support ."
}