GET /api/v0.1/hansard/entries/1456600/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1456600,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456600/?format=api",
"text_counter": 3990,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, nikirudi kwenye bajeti hii ambayo imekadiriwa, naishukuru sana Kamati ya Bajeti na Makadirio ambayo imeleta haya makadirio baada ya kuuondoa ule Mswada wa Fedha, 2024, ambayo ulikua na mambo mengi mazito mazito. Nawapongeza kwa upande wa elimu. Wameweza kuongeza Ksh247 million katika shule za msingi. Hii itawezesha watoto wakae madarasani wasome maanake tulikua tunaona hata ile dawati ya kuweza kukalia, watoto walikua wanakosa. Inabidi waendea kwa wazazi ili waweze kutengeza madawati na kuleta madarasani. Lakini katika hii bajeti, naona wameongezewa na naipongeza Kamati ya Bajeti na Makadirio kwa kazi nzuri wanayoifanya."
}