GET /api/v0.1/hansard/entries/1456606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1456606,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456606/?format=api",
    "text_counter": 3996,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "waweze pia kuangalia jambo hilo. Wakati huu hatutaki kuangalia marekebisho ya manyumba kwa sababu Wakenya wanahangaika sana na Wakenya wanataka kuangalia vitu vinavyopewa kipa umbele, viwe vitu ambavyo vitaboresha uchumi na kushika kandarasi ya kuzalisha ili uchumi uweze kuinuka na ushuru uweze kupungua. Kwa hivyo, katika hiyo pia naomba wazidi kupunguza. Licha ya sekta ya ukulima kuongezewa mgao ili iwawezeshe kukuza vyakula, Kshs100 milioni iliyotengewa Mto wa Nairobi imetolewa. Huu mto hupeleka maji sehemu kubwa za umwagiliaji maji, usafisaji na mambo mengine. Wametoa asilimia hiyo na kupelekwa katika Ofisi ya Naibu wa Rais. Ninaomba Kamati husika wairegeshe kwenye umwagiliaji wa maji katika kilimo maana ulisaidia pakubwa. Mhe. Spika wa Muda, kwenye Kitengo cha Ardhi, wameongeza Kshs750 millioni. Nimefurahi maana wakaazi wa Mombasa na sehemu ya Taita Taveta ambao walipoteza mashamba yao wako kwenye orodha ya wale watafidiwa. Pesa zimeingia sehemu husika. Watoto wetu, Gen.Z, wamefanya kazi nzuri sana. Wameamsha hili Bunge. Wameamsha bongo za waheshimiwa na sasa, zinafanya kazi. Sasa, wanaweka pesa sehemu ambazo zinakusudiwa. Nawapongeza sana. Ule mwamko ulikuwa mzuri isipokuwa waliokuwa na nia mbaya waliingilia kati. Tumepata funzo kama Wabunge na Bunge hili limeamka na kuimarika."
}