GET /api/v0.1/hansard/entries/1456609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1456609,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456609/?format=api",
    "text_counter": 3999,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "waliokuwa hawana mishahara wamepewa bajeti yao na imeongezwa. Nawapongeza. Wengi wao walikuwa wamejitolea kufunza bila malipo. Hawakuwa na mishahara. Wengi walitufuata huku wakilia ili tuwahakikishie kuwa wao pia watapata mishahara kwa kuwatetea Bungeni. Kwa sasa, watapata pesa itakayowasaidia kujimudu kiafya na kusomesha watoto wao. Kuwalipa mshahara kumenifurahisha sana. Limetua mzigo mkubwa mgongoni mwa wananchi. Kuna wakati wazazi ilibidi wachange kitu kidogo ya kuwawezesha waalimu wa JSS kupata kitu ya kujimudu. Sasa, wamepata mgao wao na mambo yao yataenda shwari. Mhe. Spika wa Muda, matibabu ya saratani katika Hospitali Kuu ya Kenyatta yamepunguziwa mgao wao. Ningependa kuwaambia wanakamati kuwa hawangeguza mgao huo. Wananchi wengi wanahangaika maana ugonjwa wa saratani hauchagui tajiri wala maskini. Ninawahisi wauregeshe maana hakuna kitu kizuri kama afya. Mengi wamefanya mazuri na nawapongeza. Naunga Mkono hii S upplementary Budget . Ofisi ya Naibu wa Rais ilikuwa na malimbikizo mengi. Nawasihi wapungunze mgao wao maana hiyo pesa waliotengewa haikuwa inaeleweka kazi yake. Hata kama wamepunguza Ksh100 millioni, nawasihi wazidi kupunguza zaidi. Yote tisa, la kumi ni kuwapongeza kwa kazi yenu nzuri. Tunaomba Nchi yetu ya Kenya iwe na amani. Tuwache vita. Hakutafanyika chochote kusipokuwa na amani. Tutakuwa kama nchi ya Sudan ama mataifa yanayopigana. Tunataka amani katika taifa letu ili tuweze kuyarekebisha yanayotutatiza tukiwa katika Jumba hili. Ahsante."
}