GET /api/v0.1/hansard/entries/1457510/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1457510,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1457510/?format=api",
    "text_counter": 547,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nilikuwa nimebofya lakini inazima ikiwaka. Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja ya kuongeza muda kwa Kamati ya Delegated Legislation ya Bunge hili ili kuchunguza na kupitisha zile kanuni za sheria za ardhi. Kanuni hizi, ijapokuwa zililetwa katika Bunge kwa muda unaofaa, lakini baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri, tukakose nafasi ya kuwasiliana na Waziri. Bw. Waziri anapaswa kuja mbele ya Kamati kujibu maswali kuhusiana na kamati hizo katika kazi ambazo tunafanya wakati tunaangalia kanuni hizo. Ukosefu wa kupatikana kwa Waziri kwa wakati imechangia pia pakubwa kuweza kukamilisha masuala haya. Kwa hivyo, muda wa siku 21 ambayo umeombwa utasaidia pakubwa kuweza kuwasiliana na Waziri. Bw. Waziri atakuja mbele ya kamati ili aweze kujibu yale maswali ambayo tulitarajia atayajibu. Pia tumeweza kupitisha kanuni nyingine tatu ambazo zilikuwa pamoja na hizo saba. Zingine nafikiri zitakuja kama ambazo zimekataliwa. Jambo la kusikitisha ni leo mchana, ripoti yetu ya zile kanuni za sheria ya afya zimekukataliwa na Bunge hili. Jambo lingine la kusikitisha ni kuwa wiki mbili zilizopita, mahakama ya majaji watatu walitupilia mbali sheria hizo za afya na ikaipa Bunge siku 120 kuweza kuangalia tena ni vipi wanaweza kuzirekebisha. Hii kwa sababu zilikuwa zinakwenda kinyume na Katiba. Kwa hivyo, ina maana kwamba sisi hapa katika Bunge mara nyingine hatuangalii ama hatuzingatii yale yanayotokea sehemu nyingine katika Serikali. Kwa mfano, ule uamuzi wa juzi wa mahakama ni kiungo muhimu kwa sababu zile kanuni ambazo tunaziangalia zilikuwa zimewekwa kwa misingi ya ile sheria ambayo imetupiliwa mbali na mahakama. Kwa hivyo, sheria imetupiliwa mbali na haiwezekani kwamba sisi kama Bunge la Seneti kuweza kuzipitisha zile kanuni. Bw. Spika wa Muda, kwa hivyo hii ni kuwatanabaisha Maseneta wezangu kwamba ni lazima tuwe macho kwa mambo yanayotendeka mahakamani. Mahakama pia inajaribu kuziangalia zile sheria ambazo tunapitisha katika Bunge hili. Ikiwa sheria ziko kinyume na Katiba, sheria hizo hazitaweza kusimama, basi tutakuwa tumepoteza wakati wetu mwingi wa kujadili na kupiga kura hapa. Hii ni kwa sababu ikifika mahakamani zinatupwa nje na tunarudi tena kuanza upya mchakato wa kuidhinisha sheria zile. Huu muda ambao tutapewa utasaidia pakubwa kuwezesha Kamati hii kukamilisha kazi yake na iweze kuleta ripoti ambayo itaeleweka katika Bunge hili. Asante."
}