GET /api/v0.1/hansard/entries/1457767/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1457767,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1457767/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu wa kuangalia mambo ya mashamba ambayo itasaidia mwananchi. Mswada huu hauhusu shule peke yake, unahusu makanisa na hata wananchi kwa sababu katika Kenya, mambo ya mashamba yameleta shida haswa kwa majimbo yetu kama vile Gatuzi la Embu, ambako mimi ninatoka. Naomba, wakati tutapata Waziri mgeni wa mashamba, mambo haya yaangaliwe ili mwananchi aweze kufurahia. Kwa mfano, katika Gatuzi la Embu, kuna shamba moja ambalo liko na mgawanyiko mkubwa kati ya kaunti na University . University inasema kwamba shamba ni lao na kaunti pia inasema shamba ni lao. Kaunti pia inasema kwamba hilo shamba liko na kazi kubwa kwa wale watu ambao wako na mbegu za kuzalisha ng’ombe ambao wananaweza kutoa maziwa mengi. Watu wa Ethics and Anti-CorruptionCommission (EACC) wametembelea hilo shamba, lakini hadi wa leo, haijajulikana kama shamba ni la university au la Kaunti ya Embu. Kwa hivyo, kama Seneta wa Embu Kaunti, kuna shida katika Embu Kaunti kama kaunti zingine. Hiyo mambo haihusu shule za msingi na sekondari pekee, yanahusu wananchi wengine. Ningeomba Serikali iweke maanani ili mambo yote iweze kuisha. Tunajuwa kuwa wananchi wengi sana wangependa kupewa cheti cha kumiliki mashamba ili waweze kukopa na pia kujenga nyumba za kukodi ili tuinue uchumi wetu wa Kaunti ya Embu. Bwana Naibu wa Spika, itawasaidia pia vijana wetu kuhamasisha familia zao kupata njia ya kufanya kazi kama ukulima au biashara zingine. Kuna wazazi wengine ambao wakipata haki ya kumiliki mashamba, wanaweza kuyauza kidogo au kufanya kazi zingine kama kutengeneza shamba, kujenga nyumba nzuri, kupanda miti na kulima. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}