GET /api/v0.1/hansard/entries/1457768/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1457768,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1457768/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Naunga mkono nikiwa Seneta wa Embu Kaunti. Tumeona kaunti nyingi. Tunaomba usajili wa mashamba uendelee vizuri. Utakuta pale Kaunti ya Embu, Manyatta Sub-County, kuna msajili anayehudumia watu wengi wanaotaka kuuza mashamba na wengine kubadilishiwa mashamba ila yule msajili anazembea na haendi kazini. Kwa mwezi, anaenda kazini siku tano. Huo mjadala uweze kuchunguza jinsi hao wasajili wa ardhi wanavyofanya kazi. Mambo mengi ya mashamba inafaa kuchunguzwa. Pale Embu Town, wanaosaidia watu kuuza mashamba wako na barua ya kufanya kazi. Utapata mtu ameelezwa kuwa shamba anayotaka ni nzuri lakini inachukua muda kwa sababu msajili haendi kazi au wanazembea kazini. Watu wa Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) watembee Manyatta Sub-County kuchunguza kazi inavyoendelea. Naunga mkono Serikali ichunguze kampuni ambazo ziko na mashamba makubwa. Kuna kampuni ya Serikali pale Kiamberee inayoitwa Tana and Athi River Development Authority (TARDA), ambayo inamiliki shamba ekari elfu kumi ilhali watu wengine hawana shamba. Kwenye hiyo amendmen t, tuone kama watu wasiokuwa na mashamba wanaweza kupata shamba kidogo. Ikiwa sio hivyo, Serikali inaweza kukodesha ekari fulani kwa miaka kama mia moja ili wengine wafaidike. Kwa kuwa Serikali inataka janga la njaa liishe, watu wa Embu wajengewe mabawa ya maji Kiamberee ili watu wapande miti, walime na kuuza mazao yao ili waweze kulipia yale mashamba. Naunga mkono kwamba mambo yaendelee vizuri. Tunafahamu kwamba Waziri atafika hivi karibuni. Tuchunguze ikiwa shida za mashamba zitaisha. Ukielekea Embu, upande wa Mwea, Makima, Karaba na pia Igamba Ng’ombe, utakuta kuna shida. Utendaji wa kazi ya wasajili wa ardhi na watu wengine iweze kulainishwa ndiposa kila mtu apate shamba lake, ajenge vizuri na kusaidia kuinua uchumi wetu wa Kaunti ya Embu. Nikimalizia, naomba msajili wa ardhi wa Manyatta sub-county achunguzwe anavyofanya kazi. Watu wengi wanataabika. Ikiwa kazi ni nyingi, tuweze kuongezewa msajili wa ardhi hapo Embu Town kwa sababu ni mmoja. Pia Surveyor hafanyi kazi inayofaa ila akifanya msajili wa ardhi anazembea kazini. Wasajili ardhi wanafaa kuwa watano. Naunga mkono ili kaunti zingine zikiendelea vizuri, pia Kaunti yetu ya Embu iendelee vizuri."
}