GET /api/v0.1/hansard/entries/1459181/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1459181,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1459181/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, ningependa kukushukuru kwa kunipa nafasi pia nichangie Taarifa ambayo imeletwa hapa na Seneta wa Meru. Bw. Spika, Judicial Service Commission (JSC) ni kati ya zile tume ambazo zinaweza kuangalia makosa yoyote ambayo mahakimu na majaji wanafanya katika kutoa hukumu zao. Kwa hivyo, ningependelea pia Kamati hiyo ya Justice, Legal Affairs and Human Rights (JLAHR) waangalie kama wanaweza kupeleka malalamishi kirasmi kwa JSC, kuhusu hukumu ya huyu Jaji ambaye amesema kwamba kazi ambayo Seneti ingefaa ifanye ipelekwe kwa Njuri Ncheke. Bw. Spika, kuna hili jambo la kwamba Jaji wa Mahakama Kuu ya Kenya, anasahau ya kwamba yule aliyechaguliwa pale ambaye ni Gavana wa Meru, amechaguliwa na watu wote wanaoishi pale Meru. Mimi ninajua kuna Pokomo, Orma na Giriama wanaoishi kule Meru. Hii ni kwa sababu watu wa Meru wanatuletea miraa sehemu ya kule kwetu na kuna watu ambao wanaenda kufanya biashara kule na wamechukua kadi zao za kura kule. Kwa hivyo, ikiwa kuna makosa ya kutatuliwa, kwa nini Jaji anafikiria wapiga kura wote wa Meru ni Wameru kwa hivyo waenda kwa Njuri Ncheke. Kuna wapiga kura pale ambao ni wa makabila tofauti. Tuna Wakisii na Wakikuyu wanaoishi Meru. Ni makosa sana kwa Jaji kusema kuwa hawa watu wote waende kwa Njuri Ncheke ambayo ni ya kabila moja. Kwa hivyo, JSC iseme jambo kuhusu hukumu. Tunaomba Kamati yetu ya JLAHR ifikirie namna tutapeleka malalamishi rasmi kwa JSC kuhusu hukumu hii, ambayo inapotosha Wakenya na kuhujumu mamlaka ya Seneti. Asante, Bw. Spika."
}