GET /api/v0.1/hansard/entries/1460323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1460323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1460323/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii kuchangia kwa mjadala wa Hoja ya ugonjwa wa kiakili ulioletwa na Mhe. Mishi Mboko. Moja kwa moja ninamuunga mkono kwa njia yoyote ile kuboresha hali ilivyo hapa nchini sasa. Ni jambo la muhimu sana. Sisi kama Wabunge, ni wakilishi wa wananchi. Jambo lolote lile ambalo litafanya mwananchi apate huduma bora, sisi hatuna budi kuliunga mkono. Kuna sababu nyingi za kusababisha haya magonjwa ya kiakili. Kuna sababu ya mihadarati, stigma, kukosa huduma pia hufanya mtu kuwa na fikra nyingi, na mambo mengine mpaka sehemu zingine tu ndio zina shida hizo. Kama kule kwetu, eneo bunge lote hakuna vituo vya burudani. Kwa mfano, uende pahali upumzike akili, inakua ngumu kwetu kule kwa sababu eneo bunge lote halina. Mambo kama haya yanasababisha vijana wetu wakafikiria mambo ya upotofu, mpaka ukaona mbona wanafanya hivi lakini kumbe sababu ni shida za kiakili."
}