HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1460325,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1460325/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "maafisa kila baada ya miaka mitatu ili mtu asikae kule zaidi. Kuna wengine ambao wanakatalia mijini kama Nairobi, Mombasa na sehemu zingine. Wenzao wanakaa msituni bila kufanya chochote mpaka wanapotea akili. Kuna sehemu inayoitwa Kiangwe; polisi akipelekwa pale, unamhurumia sana kwa sababu yeye hajazoea. Afadhali sisi kwa sababu tunaishi kule na tumezoea yale mazingira yetu. Polisi akifika pale, anakosa maji ya kuoga kwa wiki nzima. Anaweza kukaa hata bila kuoga. Wanafurahia wakati wa mvua kwa sababu wanapata maji mengi. Mvua inaponyesha, inabidi wayakusanye maji kwa muda. Kuna wakati ambapo maji yanaisha na wanabaki na ya kunywa tu. Wakati huo hawawezi hata kuoga. Sehemu hizi zikifanyiwa mpango kama huu, na kuhakikisha kwamba kila dispensary inapata mhudumu wa kushughulika na mambo haya, basi mambo mengi yatafunguka. Kwa mfano, polisi akipelekwa Kiangwe, kama hajazoea bahari, kutoka Mokowe atatumia saa moja na dakika thelathini afike kule. Akifika tu, hiyo kwake ni kama inatosha kumbadilisha akili. Kwa hivyo, lazima tuwe na mipangilio tofauti. Tusikae kwenye boardroom huku Nairobi tukipanga mipango kana kwamba Kenya yote iko kwenye meza moja. Kuna sehemu ambazo mambo ni tofauti kwa ground . Tofauti kabisa. Mimi namshukuru Rais kwa sababu siku hizi akifanya jambo, basi anafanya katika maeneo bunge yote. Kwa mfano, amesema mambo ya soko yawe katika maeneo bunge yote. Na sisi sasa tumepata imani . Jambo lingine linalosababisha mambo kufanyika hivi ni wakati mwanadamu anakosa imani. Akikosa imani anapata fikira nyingi na matatizo yanatokea. Kwa mfano, kama umekosa imani na wazazi wako, marafiki zako, na Serikali yako, basi hayo mambo huleta matatizo. Kule kwangu, kuna matatizo mengi hata wakati mwingine ninaogopa kusema. Mambo ni makubwa. Wakati mwingine, nyinyi hapa mnapokea watu wenu Bungeni, lakini wangu wanavuka wakienda Somalia na huwezi kujua sababu inayowafanya kuenda kufanya vile. Sisi huku tunawalaumu pengine wana kasoro ya akili, lakini itakuwa imechangiwa na mambo mengi. Lakini tukifanya mambo kama haya, tutadhibiti ile mienendo inayoendelea. Kama Wabunge, tunafaa kuweka sera ambazo zitasaidia watu wote sio tu wachache. Zisisaidie tu wale ambao kwao ni rahisi kufikiwa na hakuna changamoto za usafiri. Leo ninataka nichukue nafasi nishukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu Bunge sasa limeelewa kwamba Lamu Mashariki iko tofauti na maeneo bunge mengine. Ningependa kuchukua nafasi hii niseme kwamba mmeanza sasa kunielewa kwamba kuna Mbajuni na huwa ana shida. Wengi wanaelewa shida zangu sasa. Kama mfano, ungetaka kusafirisha genereta, ni lazima ingepelekwa Kiunga. Ilibidi Spika atoe onyo kwamba Mwenyekiti wa Kamati hiyo aje hapa atoe kauli. Ilikuwa inashangaza kwamba genereta ambayo ni tani saba au nane ingechukua siku mia moja na ishirini kusafirishwa. Sasa, katika huduma yeyote inayofanyika hapa Kenya, kule kwetu inakuwa ngumu kwa sababu ya changamoto ya usafiri. Mfano ni huo usafirishaji wa genereta. Huduma hizi pia zinasababisha mtu akawa na fikira. Kata nzima ya Basuba ina vijiji vitano: Basuba, Kiangwe, Mararani, Mangai na Milimani. Ukiwa huko, kufikia Level 6 Hospital, ya karibu zaidi ni hapa Nairobi, au kufikia Level 5 Hospital ni King Fahd ambayo kwa sasa wanajengewa wadi ya maternity. Hakuna mradi wowote sehemu ile. Lile eneo limebakia watu waende tu msituni kutafuta asali, na wakirudi wakae. Hizo fikira zinaweza kufanya mtu saa zingine kuchanganyikiwa na akili. Kwa hivyo, ni muhimu kila kijiji kipate hizi huduma. Nimefurahishwa sana na jambo hili. Kuna barabara moja tu ambayo ni International na Security Road . Barabara hiyo ni kwanzia Bargoni mpaka Kiunga. Ni kilomita mia moja na hamsini, lakini kwa sababu hakuna huduma, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}