GET /api/v0.1/hansard/entries/1460331/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1460331,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1460331/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Mkokoni iko ndani ya msitu. Saa hii ndio tunapambana. Mkiona tunalia hapa, mjue kwamba mambo kule ni tofauti. Katika eneo bunge nzima, barabara ambayo imejengwa kwa sasa ni ile ambayo imefanywa na Kenya Rural Roads Authority (KeRRA). Na ndio maana wakati mwingine, hatutaki mtu aitaje KeRRA. Hizi zote zinachangia mawazo mengi na ni muhimu sisi sote tufikirie kama Wakenya. Vile unafikiria kwako inakufaa, kwa mwenzako ni tofauti. Mimi nikisema kuwa ninataka polisi nikienda kwangu, mtu atashangaa sana. Kutoka Mkokoni mpaka Kiunga, ni lazima nipewe gari nzima la polisi kwa sababu ninapitia Boni Forest. Nilipokuwa Mwakilishi wa Wanawake, pesa nyingi ilikuwa ikitumika kulipa maafisa wa usalama lakini watu walikuwa wanashangaa kwa nini polisi ni wengi ilhali maafisa wawili wanatosha. Nilikuwa ninapata shida sana. Hayo mawazo yote yanachangia mambo mengi ya upotovu na kuharibika kwa akili. Asante, Mheshimiwa Spika wa Muda."
}