GET /api/v0.1/hansard/entries/1460391/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1460391,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1460391/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Mishi kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii kuhusu jambo ambalo linafaa kuangaliwa kwa makini sana. Ni haki ya kila Mkenya kupata matibabu yeyote yale kulingana na maradhi yanayompata. Maradhi ya akili yana daraja na sana sana yanaanzia katika msongomano wa mawazo. Yanaanzia mtu kusema peke yake and kuwa na uzito wa jambo fulani ambalo limemshinda kutekeleza. Inamtokea mtu anapigwa dafrau ukifikiria hakuona lakini kumbe akili yake ilikuwa haipo. Kama kila sehemu ingekuwa na zahanati katika taifa hili ambalo lina madaktari na wataalamu ambao wanaweza kushugulikia jambo hili, haya mambo yasingefikia pabaya."
}