GET /api/v0.1/hansard/entries/146044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 146044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/146044/?format=api",
    "text_counter": 318,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kuchukua nafasi hii ili kuunga mkono, Hoja hii. Nikiunga mkono Hoja hii ya makadirio ya fedha za Serikali, naomba kwanza kumshukuru na kumpongeza mwenzetu Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha, Mhe. Kenyatta, kwa makadirio ambayo amewasilisha hapa Bungeni, ambayo yanaonyesha kuwa alikariri sana na kujihusisha sana na hali ya uchumi ilivyo hapa nchini na ulimwengu wote kwa jumla. Nikichangia Hoja hii, ni mara ya kwanza ambapo tumeona makadirio ya Serikali yameelekezwa mashinani. Tukikumbuka hasa, utata tuliokuwa nao mwaka wa 2007 baada ya kupiga kura na malalamishi ambayo yalitokea, moja ya mambo ambayo yalijitokeza wazi ilikuwa ni usambazaji wa raslimali za nchi.Wananchi wengi walihisia kuwa kuna mikoa fulani ambayo, kila wakati katika makadirio ya Serikali, inapendelewa. Fedha za Serikali zilikuwa zinalenga mikoa fulani. Kwa hivyo, wananchi walikuwa na ghadhabu na ikabidi waitoe wakati huo na waeleze kinagaubaga kuwa: “Jamani, haturidhika!”"
}