GET /api/v0.1/hansard/entries/146046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 146046,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/146046/?format=api",
    "text_counter": 320,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tunashukuru kuwa Serikali wakati huu imesikia, imeelewa na imetafakari kilio cha wananchi. Imeona ni vizuri isambaze hizi hela mashinani kwa kila eneo la Ubunge ambalo limewakilishwa. Ndio hapa ninasema: Hongera kwa Serikali kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha. Hata hivyo, tunahitaji kuwa na uwazi. Fedha nyingi zimetolewa na zikapelekwa mashinani kupitia kwa CDF lakini, hata hivyo, kama ulisikia makadirio yakisomwa vizuri, kila wakati, waziri alikuwa akitaja wizara inayohusika. Swala nyeti ambalo ningependa kuliuliza hivi sasa ni: Je, kuna mikakati ambayo imewekwa wazi ya kufafanua kuwa hizo fedha zitatolewa kwa Wizara na Wizara zitafanya nini huko mashinani? Ama, tutapata hizi hela kwa vitabu na zikiingia kwa Wizara, zile shida za kila siku kama vile Katibu Mkuu au afisa fulani kutokuweko ofisini, zitaendelea? Mwaka ukiisha, tunaambiwa kuwa ijapokuwa fedha zilitolewa, imebidi zirudishwe katika Serikali Kuu kwa sababu hazikutumiwa. Ninaomba wakati huu Serikali ihakikishe kuwa fedha hizi zinatolewa hata kama zinapitia kwa Wizara, na kuwe na mashauriano ya kutosha kuhakikisha kuwa zimefanya yale ambayo yametarajiwa kufanywa katika kila eneo la ubunge. Naibu Spika wa Muda, kuna mpango wa Kazi kwa Vijana. Katika sehemu zingine, Mpango wa Kazi kwa Vijana umeanza vizuri. Lakini hakuna uwazi wa utendakazi. Hatujui hizi fedha zitatolewa namna gani, vijana wataajiriwa namna gani, watafanya kazi namna gani, watalipwa vipi na ni wangapi katika kila kiwango cha kazi. Hapo kuna swala ambalo tungependa lifafanuliwe. Nashukuru kuwa hela za hospitali zimetolewa, kitita cha Kshs20 milioni kwa kila eneo la Bunge. Kwa mfano, Hospitali ya Thesu katika eneo langu la Wundanyi imedhoofika sana. Haina mahabara, mitambo ya kupiga picha au mitambo ya kuchunguza magonjwa. Kwa hivyo, natumaini kuwa hospitali hizo zitarekebishwa na wauguzi waajiriwe. Ijapokuwa imesemekana kuwa wauguzi watakuwa wakiajiriwa kwa muda, ningeomba wakati huu, zile hospitali ambazo zimeadhirika kwa kuwa hazina chumba cha kupasulia watu na hata maji, hela hizi zitumiwe kufanya mambo hayo. Nangojea kuona ikiwa Hospital ya Thesu ambaye iko katika eneo langu la Wundanyi, itashughulikiwa vilivyo. Usambazaji wa hela mashinani umekuja wakati unaofaa ili kurekebisha barabara. Nashukuru Waziri kwa kusema kuwa zile hela ambazo zilikuwa zikitoka kwa LATF, atabadilisha sheria ili nazo ziingie katika sehemu ambazo wabunge wanawakilisha. Tutangojea kuona itakuwa namna gani. Lakini ukifikiria kidogo, utaona kuwa kuna tatizo la miundo ya misingi. Ukiangalia barabara ya kutoka Taveta kwenda Voi---"
}