GET /api/v0.1/hansard/entries/1460550/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1460550,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1460550/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Naunga mkono dada yangu, Mhe. Gladys Boss. Watu wengi sana katika nchi ya Kenya wanaugua magonjwa ya saratani kwa sababu ya yale madawa ambayo yanatumiwa katika mashamba yetu. Tusipokuwa makini, hospitali zetu zitajaa kila siku wagonjwa wa saratani. Ni dhahiri kuwa kuna watu wamejitokeza kwa kutaka kuvuna haraka. Wanatumia madawa ambayo yanaingizwa hapa kinyume na sheria kunyunyizia mimea ndani ya mashamba. Yanadhuru sana wananchi. Dadangu, Mhe. Boss, amezungumza na nakumbuka akileta mjadala huu tulivyoanza Bunge hili. Naomba tumuunge mkono na tuweke taifa ambalo litakuwa huru na maradhi ya saratani, kwa kuweza kupigia pondo huu mjadala na kuhakikisha kuwa tunaweka sheria. Tupinge na tuzuie hayo madawa yanayotolewa mataifa mengine yakiletwa hapa Kenya kunyunyizia mashamba yetu. Wale ambao wanaleta, pia wachukuliwe hatua na wafungwe. Ahsante sana dadangu, Mhe. Boss. Umekumbuka akina mama. Wengi wanalia. Hatujui ni nini ilikuwa inatuuma. Ukiingia ndani ya butchery wakati mwingine, unapata hata kuku anadungwa zile sindano. Aliyekuwa mwembamba anafura and mtu anafurahia. Lakini hajui anakula kitu gani. Kwa hivyo, nakuunga mkono. Huu mjadala upite na uwe sheria. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}