GET /api/v0.1/hansard/entries/1461830/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1461830,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1461830/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Naomba dakika zangu tatu. Nachukua fursa hii kumpongeza Rais wa taifa hili, Mhe. William Samoei Rut,o kwa kumteua ndugu wetu wa Pwani, Mhe. Hassan Ali Joho, kama Waziri wa Madini na Uchumi Samawati. Hii ni Wizara ambayo imeshika sana sehemu kubwa na uchumi mkubwa wa taifa. Naamini kuwa ueledi wake wa uongozi, vile tunavyomjua, atahakikisha kuwa madini yanaleta faida kubwa katika taifa na kuhakikisha wale watu wanaokaa sehemu ambayo tunatoa madini wanapata haki yao. Kuna wakati katika taifa hili, Mhe. Hassan Ali Joho alisimangwa. Nampongeza Kiongozi wa Chama cha Wengi kwa kusema kuwa watoto wengi hawahudhurii masomo kwa sababu ya ukosefu wa karo. Pia, kuna mambo mengi ambayo yanatoa watoto wengi darasani ndio maana hawakufanya vizuri katika masomo. Lakini hiyo haikuwa mwisho wa masomo yao. Nampongeza ndugu yangu, Mhe. Hassan Ali Joho, kwa sababu aligeuza hali yake akajisomesha mwenyewe na sasa anafanya Master’s Degree . Nina uhakika kuwa atafanya kazi kwa ueledi na kuongoza taifa la Kenya liweze kwenda mbele. Namwombea Mungu amutangulie mbele. Najua ana nguvu na uwezo wa kufanya Wizara ya Madini na Uchumi Samawati iinuke. Niruhusu niongee kuhusu huyu dada yetu, Bi. Stella, ambaye amekataliwa. Hii ni Wizara ya akina mama. Inataka Waziri ambaye anaelewa zaidi sababu gani tulipata hiyo Wizara. Ilikuwa dhahiri kuwa hakuelewa docket hiyo inahusu nini. Najua ilikuwa inatolewa katika region tofauti. Hata wale ambao wametoka kule wanaweza kutuletea mama mwingine ambaye amepigwa msasa vizuri ambaye anaweza kuhudumu katika Wizara hiyo bila kuleta sitofahamu. Kwa hivyo, hii list nyingine yote nai support . Namwomba Mhe. Hassan Joho achape kazi na kumhakikishia kuwa tuko nyuma yake. Mhe. Spika, ahsante sana."
}