GET /api/v0.1/hansard/entries/1461960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1461960,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1461960/?format=api",
"text_counter": 404,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Nimesimama hapa kuunga mkono haya majina yote ya watu ambao wameteuliwa na Rais William Samoei Ruto ili wawe mawaziri. Tunashukuru kama wanawake kwa sababu wanawake watano wameweza kupatiwa nyadhifa kubwa mbali mbali. Hii ni haki yetu sisi kama wanawake. Vile vile, tunashukuru kwa sababu tumeona kijana moja ambaye ameteuliwa kuongoza Wizara ya Maji. Sisi kama vijana pia hili jambo limetufurahisha. Ningetaka kuwaambia wale mawaziri ambao wameteuliwa mambo mawili. Jambo la kwanza ni kwamba hatutaki watu wa ‘Yes, Sir ’ . Tunataka watu ambao wataketi na Rais na kumsaidia ili Kenya iweze kusonga mbele. Hawa watu watakuwa karibu sana na Rais na hawafai kuwa watu wa ‘Yes, Sir. ’ Wanafaa wawe watu ambao watamsaidia Rais. La pili, ni kwa wale mawaziri ambao wamekuwa ofisini kwa miaka miwili lakini, kwa sababu ambazo hazingeweza kuepukika, wameachishwa kazi, hata hawa ambao wamepatiwa kazi wajue kwamba Wakenya wako chonjo na wasipofanya kazi yao vizuri, Wakenya wataanguka na wao. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}