GET /api/v0.1/hansard/entries/1461969/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1461969,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1461969/?format=api",
    "text_counter": 413,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kasim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kusema kwamba siungi Ripoti hii mkono pekee, bali naiunga pamoja na miguu, kichwa, nywele, macho na kila kitu changu. Kwa sababu hakuna siku ambayo Kamati imeweza kufanya kazi nzuri kama hii na kutoa Ripoti yake bila kushawishiwa na mtu kuona kwamba huyu anafaa ama hafai. Yule ambaye wanakamati waliona hafai, walitamka hivyo. Nachukua fursa hii kumshukuru Rais kwa kumteua kwa mara ya pili aliyekuwa waziri mstahiki Gavana wa kwanza wa Kwale Mhe. Salim Mvurya. Kutokana na kazi ambayo aliifanya, nina amini kuwa katika zile memoranda ambazo zilipelekwa, hakukuwa na hata moja ambayo ilikuwa inamkashifu Waziri Salim Mvurya. Licha ya kuwa alikuwa amehudumu kama waziri kwa kipindi cha karibu miaka miwili, pato lake bado liko chini ya Ksh200 milioni. Hili limekuwa jambo la kushangaza kwa Wakenya. Wanajiuliza, wakati mawaziri wengine kwa muda huu mfupi wameweza kujilimbikizia Ksh300 milion na zaidi, mbona yeye bado hajapata hata zaidi ya Ksh100 milioni? Na hili linaweka wazi kwamba yeye ni mwadilifu, anafanya kazi kwa kutambua Wakenya na hilo ndilo jukumu la mawaziri. Pia, nichukue fursa hii kushukuru kuteuliwa kwa Mhe. Hassan Joho, ambaye amepatiwa ile wizara changa, lakini ina matumaini makubwa katika kuboresha uchumi wa Kenya. Siyo watu wa Pwani peke yao walio na Bahari Hindi, lakini ina nafasi ya kuajiri na kuleta fedha nyingi katika hii nchi ya Kenya. Vilevile, nina imani kwamba Waziri aliyeteuliwa ana tajiriba ya kuweza kufufua wizara hiyo na kuleta mapato makubwa. Ahsante, Mhe. Spika."
}