GET /api/v0.1/hansard/entries/1462268/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1462268,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462268/?format=api",
    "text_counter": 116,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono ile Taarifa iliyoletwa na Seneta kutoka Meru, Sen. Kathuri. Kuna mikataba kati ya gatuzi zetu na madaktari kuhusu vile ambavyo matibabu yatakua yakielekezwa. Mikataba hii ni kama haina faida ya kukamilishwa ama wale wanaandika hii mikataba hawana haja ya kukamilisha. Ndio maana kila saa unapata kuna migomo katika hospitali zetu. Wananchi wa gatuzi zetu wanafanya vile inapaswa. Unapata mtu amelipia bima ya NHIF, lakini akienda hospitali, hakuna dawa. Nikiunga Taarifa hiyo, saa zingine inafika wakati ninakisia vile wananchi wengi wa Kenya wanavyosema, kwamba ni vizuri afya ama matibabu irudishwe kwa Serikali Kuu. Gatuzi zimezembea kwa kazi zao. Muhula uliopita, madaktari katika Kaunti ya Laikipia na Kirinyaga waligoma wote. Hakuna kitu kinaendelea kwa sababu ukiandikiwa dawa katika hospitali zetu, nimesikia Sen. Chute akisema unaambiwa uje na maji, sindano na kila kitu. Ni kama hospitali yenyewe ni jengo tu na wewe unapaswa kuja na kila kitu. Bi. Waziri wa Afya aliyeteuliwa yuko na uzoefu kama vile Gen Z walivyosema. Sasa tumeteua daktari aliye na uzoefu. Sasa tunataka tumwone Dkt. Baraza akifanya ile kazi aliyoteuliwa kufanya angalau Wakenya wapate afueni."
}