GET /api/v0.1/hansard/entries/1462269/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462269,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462269/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Kuna Taarifa iliyoletwa na Sen. Asige. Nilitazama mashindano kule Paris Wakenya wakikimbia. Niliona msichana anayeitwa Yavi na aliyetoka Makueni. Nikiangalia mitandaoni, niliona Yavi akisema ya kwamba kisa na maana cha yeye kutowakilisha nchi yetu ni kuwa aliitishwa zaidi ya Kshs200,000. Hawezi pata pesa kama hizi. Lakini anaendelea kusema hata baada ya ufisadi ulio katika Wizara, alijikakamua na akaingia katika nchi ile. Bw. Spika, ninajua ya kwamba, Mhe. Kipchumba Murkomen ambaye tumekuwa na yeye hapa na mwenye kupewa hio Wizara, atawajabika. Nilitazama nikijua sisi tutafuzu sababu hizo mbio kila wakati tumekuwa tukifuzu. Lakini, niliona wakimbiaji wa Kenya wakishindwa na wakimbiaji wa nchi zingine. Nilidhania wale watu wangetushinda katika ndoto, lakini sasa, ilikuwa ikitendeka. Kwa hivyo, Waziri wa Afya na Waziri wa Michezo walioteuliwa, na kazi chungu nzima. Ningependa kumrudishia Seneta Syengo shukrani kwa yale ambayo amefanya na tunamwambia heko na aendelee vivyo hivyo, kwa sababu, umoja ni nguvu, utengo ni udhaifu."
}