GET /api/v0.1/hansard/entries/1462299/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462299,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462299/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa kadhaa. Taarifa ya kwanza imeletwa na Sen. Cherarkey kuhusu biashara ya majani chai katika soko la Mombasa. Hapo awali, Bunge la Seneti lilipitisha kanuni ambazo ziliipatia Serikali mamlaka ya kuweka bei ya majani chai chini. Kutokana na kanuni hizo, uuzaji wa majani chai umedorora kwa sababu majani chai hayauzwi kulingana na mahitaji ya soko. Bei katika soko huru inapatikana kutokana na wingi wa majani chai na upungufu wa haja yaani demand and supply factors . Kuweka bei ya kudumu ya chini ya majani chai imefanya soko kudorora. Mara nyingi, majani chai yanapouzwa hayawezi kupata ile bei ya chini kabisa ambayo soko imeweka. Kuna majani chai ambayo yanakuja katika soko kupitia Kenya Tea Development Agency (KTDA) na vile vile kutoka watu binafsi. Majani chai ambayo yameleta matatizo ni yale yanatoka kwa shirika la KTDA. Swala hili litaweza kutatuliwa iwapo zile kanuni zinazosema kuwe na bei ya chini ya majani chai itabadilishwa ili kuhakikisha soko liko huru. Swala hili linafaa kutatuliwa na East African Tea Trade Association (EATTA) ambalo linasimamia soko hili, ili waangalie ni vipi watadhibiti bei ya majani chai ili yasipate bei ya chini. Bi. Spika wa Muda, vile vile, ningependa kuchangia Statement ya Sen. Crystal Asige kuhusu kudorora kwa Team Kenya katika michezo ya olimpiki ya mwaka huu inayofanyika hivi sasa mjini Paris. Tumekuwa tukijipa kipao mbele kwa maswala ya michezo hususan riadha. Tulikuwa na uhakika tutapata medali ya dhahabu katika mbio za mita 800, 1,500, 3,000 vya kuruka maji na vuizi, 5,000, 10,000, marathon na vile vile kutembea kilomita 20."
}