GET /api/v0.1/hansard/entries/1462300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462300,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462300/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Mpaka sasa, tumepata medali moja ya dhahabu pekee katika mbio za mita 1,500 za wanawake. Haya ni matokeo duni sana kulingana na vile ambavyo tumekuwa tunafanya katika michezo hii. Haya yametangamana na udhaifu wa Serikali kuwekeza kikamilifu kwa michezo hii. Tumeona mkimbiaji kama Faith Kipyegon akishinda mbio nyingi hapo nyuma. Aliweka na kumiliki rekodi nyingi za ulimwengu nafikiri katika mbio za mita 1,500 na 5,000. Yeye ndiye mmiliki wa rekodi ya dunia. Lakini, juzi hakuweza kufua dafu. Labda alikuwa amechoka au kuumia akijaribu kufikia kiwango kile cha michezo ya Olimpiki. Tungependa kuwe na uwazi wa uchunguzi wa matokeo haya duni. Vile vile, kuwe na mfumo wa kuboresha hali yetu ya michezo. Tutaiboresha michezo hii wakati tutaweka stadia au viwanja vya kisasa vitakavyotumiwa na wachezaji wetu. Bi. Spika wa Muda, tumepiga kelele hapa kwenye Bunge kuhusu swala la Football Kenya Federation (FKF) - Mpira wa kandanda. Mwaka jana, tulifanya mikutano kadhaa na FKF pamoja na Waziri aliyeondoka, Mhe. Ababu Namwamba. Mpaka sasa, hali ni ya utata. Mahakama ilisema kuwa ofisi ya Mr. Nick Mwendwa imemaliza muda wake lakini bado yupo pale pale. Hajaitisha mkutano mkuu wa mwaka ili kupanga mikakati ya kuchagua atakaye miliki ofisi ile. Hatuwezi kukaa hivi wakati hali yetu ya michezo inadorora. Nilifurahi juzi wakati ambapo Mheshimiwa Murkomen alikuwa anahojiwa na kusema kwamba atahakikisha amesafisha mashirika yote ya michezo. Alisema pia kuwa ameona kila mara Serikali ikitaka kuchukua hatua kwa mambo ya kandanda kila mtu anaikimbilia Fédération Internationale de Football Association (FIFA). Hii ni Taarifa nzuri lakini sasa ni wakati wa kuibadilisha kuwa vitendo. Mheshimiwa anafaa aanze na FKF na ahakikishe kuwa tumepata uongozi mpya kufikia Desemba mwaka huu ili matayarisho ya Africa Cup of Nations (AFCON) 2027 yawe sawa sawa ili Kenya ifanye vizuri katika michezo hiyo. Ni jambo la kusikitisha kwamba mpaka sasa hatuna kiwanja ambacho kinaweza kutumika kuaandaa michezo inayodhaminiwa na shirika la FIFA ulimwenguni au Confederation of African Football (CAF). Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Statement ambayo imeletwa na Sen. Crystal Asige. Sote tunahudumu katika Kamati ya Leba na Maswala ya Jamii katika Bunge hili."
}